Mojim Lyrics
Mojim Lyrics > Americas singers > Leteipa the King > Fuliza > Fuliza

Leteipa the KingLyrics
Album list

Leteipa the King

Fuliza

ft DreamBoy

Verse {Leteipa the King}:
Nilikutunza kama mboni,
Kama walenje mfukoni,
Nilikupenda sana Wewe, Kisha ukaniacha mwenyewe,
Kidonda changu hakiponi,
Nakutafuta sikuoni,
Kumbe ulibebwa na mwewe, ukaniachia kiwewe,
Na kale kamia,
Ulinitupia
Sijakatumia bado nakaangalia
Nikifikiria vile ulinichukulia
Kama sufuria ama kama ligunia
Nilikupa kila kitu, vya nje mpaka vya ndani,
Nawe ukanipa jipu, kupona Mi sidhani,
Ni kweli nahisi wivu, kukuona kwa Fulani,
Penzi lishakuwa jivu, kuni ziliisha zamani,

Chorus {Leteipa the King}:
(Nine choke kuwa nawe,) my confidence
( nawe ,) my self esteem
(nawe , ) my holyness
(nawe,) My future dream
(Nawe) My only space,
(Nawe) My golden blings
(Nawe) Zote umezifuliza
(Nimechoka kuwa Nawe) Nirudishie ring yangu
(Nawe) hata kambuzi ketu kana kidole
(Nawe) bora nidate simu tangu
(Nawe) itanitreat better nipone

Verse 2 {DreamBoy}:
Find more lyrics at ※ Mojim.com
Nilikuenzi ka Kiba kwa Cinderella
Nikakupa penzi, kumbe ulichojali ni hell
Nikuhonge benz , magari ka ya telenovela
Na sina Centi kapuku kama mfungwa jela
Ila moyo wangu Nilikupa uniwekee
Ukaondoka na kuniachia upweke
Heartbroken moyoni Mi niteseke
Huku na kule Beshte zako wanicheke
{Leteipa the King}
Na kale kamia,
Ulinitupia
Sijakatumia bado nakaangalia
Nikifikiria vile ulinichukulia
Kama sufuria ama kama ligunia

Chorus {Leteipa the King}:
(Nine choke kuwa nawe,) my confidence
( nawe ,) my self esteem
(nawe , ) my holyness
(nawe,) My future dream
(Nawe) My only space,
(Nawe) My golden blings
(Nawe) Zote umezifuliza
(Nimechoka kuwa Nawe) Nirudishie ring yangu
(Nawe) hata kambuzi ketu kana kidole
(Nawe) bora nidate simu tangu
(Nawe) itanitreat better nipone
(Nimechoka kuwa nawe) kweli Haya ni mapenzi ama uhusiano wa kibiashara
(Nawe) Kila mwisho wa mwezi nikupe tayari kukupa mshahara
(Nawe) Nimechoka siezi tazama mwenzako nilivyoparata
(Nawe) Miaka yangu Ni michache lakini tayari nishatoka kipara